1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Shambulizi la bomu Irak limeua watu 8

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CN

Watu 8 wameuawa katika mripuko wa bomu uliotokea Jisr Diyala,kusini-mashariki ya mji mkuu wa Irak, Baghdad,wanakoishi Washia wengi.Wengine 13 pia wamejeruhiwa.Maafisa 2 wa polisi na wanawake 2 ni miongoni mwa majeruhi.Maafisa ambao hawakutaka kutajwa kwa jina wamesema,shambulizi hilo lililenga mkahawa unaotumiwa na watumishi wa serikalini na wafanyakazi wa ujenzi.Jumatano iliyopita,shambulizi la bomu katika eneo hilo hilo,liliua watu 8 na wengine 24 walijeruhiwa.