1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD : Wairaq watakiwa kuungana

13 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCAD

Viongozi kutoka kote nchini kote Iraq iliogawika na mfarakano wa kimadhehbu wametowa wito wa kuwepo kwa umoja katika kikao maalum cha bunge leo hii chini ya ulinzi mkali kulaani shambulio la kujitolea muhanga maisha dhidi ya jengo la bunge.

Msemaji mwandamizi wa serikali amesema mafisa wa serikali walikuwa na taarifa za ujasusi na mapema kwamba wanamgambo walikuwa wakipanga kulishambulia bunge kabla la shambulio hilo la jana ambalo limemuuwa mbunge mmoja na kujeruhi watu zaidi ya 20 kwenye mkahawa wa bunge hilo.

Wafanyakazi watatu wa mkahawa wa bunge hilo lenye ulinzi mkali wamekamatwa na baadhi ya walinzi wa bunge pia wamekuwa wakichuchunguzwa lakini hakuna anaeshikiliwa.

Awali jeshi la Marekani lilisema kwamba watu wanane wamejeruhiwa katika mripuko huo wakiwemo wabunge watatu.