1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD. Wanajeshi watatu wa Marekani wauwawa

2 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6s

Jeshi la Marekani limetoa taarifa kuwa wanajeshi wake watatu wameuwawa wakati wa operesheni katika jimbo la magharibi mwa mkoa wa Anbar.

Wanajeshi wawili waliuwawa na maadui na mmoja ameuwawa kufuatia ajali ya gari.

Wakati huo huo polisi nchini Irak imegundua takriban maiti 50 zilizotupwa katika maeneo ya mji mkuu wa Baghdad usiku wa jana.

Miili ya watu hao ilikuwa na majeraha ya risasi na inakisiswa kuwa vifo hivyo vinatokana na vita vya kijamii vinavyo kithiri katika mji wa Baghdad baina ya Wassuni na Washia.