1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wanamgamboi wa Al-Qaeda wameuawa Iraq

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBp4

Vikosi vya Marekani na Iraq vimewakamata wanamgambo 2 wa Al-Qaeda wa ngazi ya juu na wapiganaji wengine 7 katika wilaya ya Diyala. Azma ya operesheni hiyo ya majeshi ya Marekani inayoendelea kwa siku ya tano,ni kuwateketeza waasi waliojificha Diyala.Jeshi la Marekani pia limesema kuwa katika uvamizi uliofanywa kwengineko nchini Iraq,wapiganaji wengine 7 wa Al-Qaeda wameuawa na washukiwa 10 wamekamatwa katika miji ya Tikrit,Fallujah,Baghdad na Mosul. Katika operesheni nyingine ya uvamizi ukingoni mwa Baghdad,katika mtaa wa Sadr City,wanakoishi Washia wengi zaidi,wanamgambo 3 walizuiliwa. Katika tukio tofauti,watu wenye bunduki walivamia jengo la shule linalotumiwa na vikosi maalum vya Iraq katika mji wa Samarra,ulio kaskazini mwa nchi.Maafisa 2 wa polisi waliuawa na wengine 6 walijeruhiwa katika shambulio hilo.