1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Wasunni wajitoa serikalini.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBd4

Kundi kuu la kisiasa la Wasunni nchini Iraq limesema kuwa linajiondoa kutoka serikali ya mseto ya nchi hiyo kwasababu ya kushindwa kwa waziri mkuu Nouri al – Maliki kukubali orodha ya madai yao kadha.

Hatua hiyo ni pigo kwa serikali ya umoja wa kitaifa inayoongozwa na al - Maliki na inatarajiwa kuleta mvutano katika mazungumzo baina ya jamii kubwa ya Washia nchini humo na makundi ya Wasunni ambao ni wachache.

Marekani imekuwa ikiitaka serikali ya Iraq kukubaliana na sheria kadha zenye lengo la kushughulikia wasi wasi wa Wasunni na kupunguza ghasia za kimadhehebu.

Wakati huo huo , mashambulizi kadha ya mabomu ya kijitoa muhanga mjini Baghdad, yamesababisha vifo vya kiasi cha watu 50 na wengine kadha kujeruhiwa.