1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD: Wateka nyara watoa agizo jipya

3 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCCy

Wateka nyara nchini Irak wanao mshikilia mateka mwanamke mmoja wa Kijerumani na mwanawe wametoa agizo jipya kwa serikali ya Ujerumani.

Wateka nyara hao wameitaka Ujerumani ianze kuwaondoa wanajeshi wake kutoka nchini Afghanistan katika muda wa siku kumi la sivyo mateka hao watauwawa.

Katika picha ya video kupitia mtandao wa internet wa kiislamu mwanamke huyo mwenye umri wa mika 61 Hanelore Krause anaiomba serikali ya Ujerumani itekeleze agizo la wateka nyara hao.

Bibi Krause alitekwa nyara na mwanae mwenye umri wa miaka 20 mjini Baghdad miezi miwili iliyyopita.

Hili ni agizo la pili kutolewa na wateka nyara hao kwa serikali ya Ujerumani.

Wakati huo huo takriban watu 12 wameuwawa na wengine 150 wamejeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika mji wa Kirkuk kaskazini mwa Irak.

Mlipuaji huyo wa kujitoa muhanga alijilipua ndani ya gari alilokuwa akisafiria karibu na kituo cha polisi.

Taarifa za polisi zinaeleza kuwa shambulio hilo limefanyika sambamba na ziara ya wanajeshi wa Marekani waliokuwa wamekitembelea kituo hicho cha polisi.