1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad. Watu wanane wauwawa kwa bomu.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HA

Bomu lililokuwa katika gari limelipuka katika eneo la biashara katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad , na kuuwa kiasi watu wanane na kuwajeruhi wengine 25, ikiwa ni pamoja na polisi wa barabarani wanne.

Katika kitongoji kinachoishi Washia cha Shaab mjini Baghdad, gari nyingine iliyowekwa milipuko , imelipuka na kuuwa watu wawili na kuwajeruhi wengine 16.

Hapo mapema mabomu mawili katika magari katika mji wa kaskazini wa Baiji yamesababisha vifo vya watu 14 na kuwajeruhi wengine 30. Mashambulio hayo yamekuwa miongoni mwa wimbi la mabomu katika siku za karibuni wakati juhudi za kigaidi za kundi la al-Qaeda zinachukua kasi wakati mwezi mtukufu wa Waislamu unakaribia mwisho.