1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad: Waziri mpya wa ulinzi wa Marekani aizuru Irak

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChe

Siku mbili baada ya kuapishwa kuwa waziri mpya wa ulinzi wa Marekani, Robert Gates yuko Baghdad kukutana na makamanda wa jeshi la Marekani na kujionea mwenyewe vita hivyo ambavyo anasema Marekani haishindi wala haishindwi. Ziara ya Waziri Gates mwenye umri wa miaka 63 na mkurugenzi wa zamani wa Shirika la ujasusi la Marekani CIA, inafuatia ripoti mpya ya wizara ya ulinzi kwamba machafuko nchini Iraq yako katika kiwango cha juu kabisa wakati idadi ya wanajeshi wa Kimarekani waliouwawa ikikaribia 3,000 . Awali ikulu mjini Washington ilithibitisha kwamba rais George W. Bush anazingatia kuongeza wanajeshi kwa kipindi kifupi nchini Irak. Hivi sasa kuna kiasi ya wanajeshi 140,000 wa Marekani nchini humo.