1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:amri ya kudhibiti usalama yaondolewa Baghdad

18 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqk

Amri ya kudhibiti usalama , iliyotumika kwa muda wa siku nne imeondolewa katika miji ya Baghdad na Basra kusini mwa Irak. Amri hiyo ilitangazwa baada ya msikiti wa washia kushambuliwa kwa bomu katika mji wa Samarra.Shambulio hilo lilifuatiwa na jingine kwenye msikiti wa wasuni katika mji wa Basra.

Wakati huo huo Marekani imetaarifu kuwa askari wake watatu wameuawa kutokana na mabomu yaliyotegwa njiani. Wawili waliuawa mjini Baghdad na mwengine katika jimbo la Kirkuk.

Hatahivyo taarifa ya jeshi la Marekani imesema kuwa majeshi yake kwa kushirikiana na ya Irak sasa yanadhibiti asilimia 40 ya mji wa Baghdad.