1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad:Hujuma za Wamarekani zauwa watu 13 mjini Sadr.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Dr

Hujuma za ndege za kijeshi za Marekani asubuhi ya leo katika mji wa Sadr nchini Irak,zimewauwa kiasi ya watu 13 na kuwajeruhi wengine 52. Duru za polisi zimesema miongoni mwa waliouwawa ni wanawake na watoto. Duru moja wapo ilisema hujuma hizo za Marekani zilifanywa baada ya gari moja ya jeshi la Marekani kushambuliwa kwa bomu lililotegwa kandoni mwa barabara. Wilaya hiyo ya Sadr ni ngome ya wanamgambo wa Mehdi waliyo watiifu kwa Kiongozi wa kidini Moqtada al-Sadr na kimegeuka kituo cha mapigano ya mara kwa mara kati ya majeshi ya Marekani na wanaharakati wa kishia.