1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Miripuko ya bomu imeua watu 70 nchini Irak

17 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCa4

Hadi watu 70 wameuaua nchini Irak katika miripuko miwili iliyotokea katika chuo kikuu mjini Baghdad.Stesheni ya televisheni ya Irak imesema, mshambuliaji aliejitolea muhanga alijiripua wakati mmoja na bomu lililotegwa kwenye gari, wakati ambapo wanafunzi wa chuo kikuu cha Mustansiriyah walikuwa wakingojea kupanda mabasi. Zaidi ya watu 160 pia walijeruhiwa katika shambulio hilo,likiwa ni moja kati ya mfululizo wa mashambulio yaliotokea siku ya Jumanne katika mji mkuu Baghdad.Hapo awali,Umoja wa Mataifa ulitoa ripoti juu ya idadi ya watu waliopoteza maisha yao mwaka jana nchini Irak.Kwa mujibu wa ripoti hiyo,zaidi ya watu 34,000 waliuawa nchini humo katika mwaka 2006,hiyo ikiwa ni wastani wa kama watu 94 kuuawa kila siku moja.