1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Mshukiwa mmoja azuiliwa kwa tuhuma za kufadhili ugaidi

4 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7If

Majeshi ya Iraq na Marekani yanamzuia mtu mmoja anayeaminika kupokea dola milioni laki moja katikati ya mwaka huu kutoka kwa wanaounga mkono shughuli za kundi la kigaidi la Al Qaeda kwa madhumuni ya kufadhili vitendo vya ugaidi nchini Iraq.Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la Marekani nchini Iraq mtu anayezuiliwa mjini Baghdad katika mtaa wa Al Kindi anashukiwa kulipa kundi la Al Qaeda dola alfu 50 kila mwezi na kutumia biashara yake ya bidhaa za ngozi kama kisingizio.

Mtu huyo aidha anashukiwa kusafiri nchi za nje kutafuta pesa za kuwapa kundi hilo na kuajiri watu walio na msimamo mkali kusaidia kusafirisha mali ghafi ya kutengeza mabomu.mabomu hayo yanapangwa kutumiwa na wanamgambo kushambulia majeshi ya muungano yanayoongozwa na Marekani.

Jeshi la Marekani pia linamlaumu mshukiwa huyo kuhusika na mashambulizi mawili katika msikiti mtukufu wa Kishia unaozua mvutano mkubwa katika ghasia zilizo na misingi ya kidini nchini Iraq.

Mtu huyo anahusishwa na ununuzi wa zana za kulipuka na silaha zilizotumika katika shambulizi la mwezi Februari mwaka jana kawenye msikiti wa Al Askari mjini Samarra.Kulingana na jeshi la Marekani nchini Iraq mshukiwa huyo ana maduka nchini Jordan,Syria na mjini Fallujah ulioko Iraq..Anasakwa kwa madai ya kuwapiga risasi wanajeshi 3 wa Marekani na kujeruhi mwengine mmoja mwezi Aprili mwaka huu.