1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Wanajeshi saba wa Marekani wauawa

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC08

Wanajeshi saba wa Marekani wameuawa pamoja na mfasiri mmoja katika mashambulizi tofauti huko Iraq

Hapo jana askari sita wa Marekani wakiwa na mfasiri wao waliuawa, baada ya msafara wao kushambuliwa kwa bomu huko Magharibi mwa Baghdad.

Maperma askari mmoja wa Marekani aliuawa na wengine watatu kujeruhiwa baada gari lao kushambuliwa kusini mwa Baghdad.

Mauaji hayo yanafanya idadi ya askari wa Marekani waliyouawa huko Iraq toka siku ya Ijumaa kufikia 15 na 76 toka mwezi huu uanze.

Wakati huo kumesikika milipuko katika eneo lenye ulinzi mkali wa majeshi ya Marekani la Green Zone katikati ya Baghdad, lakini hakuna taarifa zaidi.