1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD.Wanajeshi watano wa Marekani wauwawa

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwP

Jeshi la Marekani limetoa taarifa kwamba wanajeshi watano zaidi wameuwawa nchini Irak.

Zimebakia siku nne kabla ya kufanyika uchaguzi wa kati nchini Marekani huku vita vya Irak vikigubika kampeni za uchaguzi huo.

Wakati huo huo polisi nchini Irak imesema kuwa imegundua maiti 55 katika muda wa saa 24.

Katika mwezi wa oktoba pekee wajeshi 105 wa jeshi la Marekani waliuwawa nchini Irak.