1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Watu 13 wanyongwa

20 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChw

Maofisa nchini Iraq wametekeleza adhabu ya kifo kwa kuwanyonga watu 13 waliopatikana na hatia ya kuua na utekaji nyara.

Hatua hiyo ya aina yake imekuja wakati ambapo kuna ongezeko la ghasia katika mji mkuu Baghdad.

Tukio hilo pia limeonyeshwa kwenye vyombo vya habari nchini humo.

Mtu mmoja ambaye pia alikuwa miongoni mwa watuhimiwa hao 13 ilisika akiambiwa na maafisa waliokuwa wakitekeleza adhabu hiyo kwamba rufaa yake imekataliwa na mahakama na hivyo inabidi auwawe.

Picha za tukio kama hilo ni nadra kuonyeshwa katika televisheni ya Iraq tangu kung’olewa madarakani Saddam Hussein na hata wakati wa utawala wake licha ya adhabu hiyo kutekelzwa lakini haikuwa kawaida kuonyeshwa hadharani.