1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baghdad.Watu kadha watekwa nyara katika wizara ya fedha.

30 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwh

Watu waliokuwa na silaha wakivalia sare za jeshi la polisi wamewateka nyara kundi la raia wa mataifa ya magharibi kutoka katika wizara ya fedha.

Ofisi ya wizara ya mambo ya kigeni mjini London imethibitisha kuwa Waingereza watano ni miongoni mwa watu waliotekwa.

Polisi wamesema kuwa watu hao waliokuwa na silaha waliwasili wakiwa katika mlolongo mrefu wa magari, ambayo kwa kawaida hutumika na polisi, na kufunga eneo lote pamoja na mitaa kuzunguka jengo hilo kabla ya kuwachukua mateka wao.

Kwingineko mjini Baghdad, mabomu mawili yaliyokuwa katika magari yamesababisha vifo vya kiasi watu 38 na kuwajeruhi wengine 60.

Na Marekani imesema kuwa vifo vya wanajeshi wake 10 juzi Jumatatu vimefanya mwezi huu kuwa mbaya zaidi kwa majeshi ya Marekani katika muda wa miaka miwili na nusu iliyopita.