1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAKU. Upinzani nchini Azerbaijan wajiandaa kufanya maandamano

7 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKm

Upinzani nchini Azerbaijan umesema unajiandaa kufanya maandamano makubwa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa bunge uliofanyika hapo jana nchini humo. Maandamano hayo yanatarajiwa kuanza hapo kesho katika mji mkuu wa nchi hiyo, Baku, katika juhgudi za kuyapinga matokeo ya uchaguzi ambayo upinzani unasema yalikuwa na udanganyifu.

Tume ya uchaguzi nchini humo ulikitangaza chama tawala kuwa mshindi wa uchaguzi wa jana. Chama chake rais Ilham Aliyev kimesema hapakuwa na dosari nyingi katika uchaguzi huo. Waangalizi wa mataifa ya magahribi wanatajiwa kutoa taarifa yao baadaye.