1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bangladesh: Vita dhidi ya mihadarati vyapamba moto

Saumu Mwasimba
29 Mei 2018

Zaidi ya washukiwa 100 wameuwawa na maelfu kukamatwa katika kipindi cha wiki mbili: Mauaji hayo ni mtindo unaoshuhudiwa nchini Ufilipino katika mapambano dhidi ya mihadarati ,Wasiwasi kuhusu haki za binadamu umeongezeka

https://p.dw.com/p/2yUze
Bangladesch Dhaka Polizei in Lieferwagen mit verhafteten politischen Aktivisten
Picha: bdnews24.com

Polisi inasema kwamba washukiwa kumi zaidi wanaodaiwa kuhusika na usafirishaji haramu wa dawa za kulevya walipigwa risasi mapema asubuhi ya jumanne baadhi wakiuwawa baada ya kupigwa risasi na polisi na wengine wakiuwawa katika kile kilichotajwa kuwa vita kati ya wafanyabiashara wa mtandao wa madawa ya kulevya. Washukiwa jumla ya 102 wa kusafirisha madawa ya kulevya wameuwawa tangu Bangladesh ilipoanzisha mapambano makubwa dhjidi ya madawa ya kulevya katikati ya mwezi Mei yanayolenga kuisambaratisha kabisa biashara hiyo inayoongezeka nchini humo.

Waziri wa mambo ya ndani Asadduzzaman Khan ameliambia shirika la habari la AFP kwamba wanasimama kidete kuona vita hii inaendelea hadi pale watakapofanikiwa kuidhibiti kabisa. Washukiwa kiasi 12,000  wamekamatwa na kushtakiwa katika mahakama maalum tangu yaliypoanzishwa mapambano ya kuwaandamana wanaohusika kuuza na kusafirisha madawa ya kulevya mnamo Mei 15 huku wengi wa watuhumiwa wakikutikana na hatia na kuhukumiwa vifungo kati ya siku saba hadi miezi sita jela.

Bangladesch - Zahlreiche Todesvolle durch Razzien gegen Drogenhandel
Picha: bdnews24

Kwa mujibu wa waziri Khan waliouwawa katika vita hivyo hapana shaka walikuwa ni wafanyabiashara kabisa wa madawa ya kulevya  licha ya kutolewa madai na makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba watu wasiokuwa na hatia ndio waliouwawa. Hata hivyo waziri huyo wa mambo ya ndani anasisitiza kwamba waliouliwa ni watu waliokuwa na bastola  na walidiriki kufyetua risasi mara tu walipowaona polisi,na huo ni ushahidi tosha ulioonesha kwamba walikuwa sio watu wazuri .

Bangladesch Razzia gegen Islamisten
Picha: bdnews24.com

Tume ya kutetea haki za binadamu nchini humo hata hivyo wiki hii imezungumzia wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na kuongezeka idadi ya wanaouwawa na kutoa tahadhari kuhusu mauaji yanayofanywa kiholela bila kuzingatia sheria. Kikosi maalum cha mapambano dhidi ya madawa ya kulenya kimesema watu 24 waliouwawa na polisi wa kikosi hicho walikuwa ni vinara katika mtandao wa biashara ya mihadarati ingawa pia kikosi hicho hakijatowa ushahidi wa hilo.

Miongoni mwa waliouwawa inatajwa yupo pia diwani kutoka jimbo la Teknaf ambaye wafuasi wake wanasema hakuwa na maingiliano yoyote na madawa ya kulevya. Kwa upande mwingine waliouwawa leo Jumanne walikuwemo pia washukiwa wawili wanaodaiwa kuwa vinara wakuu wa mtandao wa biashara hiyo ambao walikutwa na polisi tayari wameshauwawa baada ya kutokea kile kinachoelezwa kwamba ni vita baina ya makundi mawili ya mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya katika mkoa wa Jessore. Bangladesh imekuwa ikipambana kuithibiti biashara hiyo haramu katika eneo la yaba huku mamilioni  ya vidonge vya madawa ya kulevya  vikiingizwa nchini humo kutokea Myanmar.serikali inasema mwaka jana inakadiriwa vidonge milioni 40 vya madawa ya kulevya vinavyoitwa yaba viliingizwa sokoni nchini humo.

Mwandishi:Saumu Mwasimba

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman