1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAQUBA: Washukiwa 17 wa Al-Qaeda wauawa Iraq

22 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBpN

Nchini Iraq,watu 17 wanaoshukiwa kuhusika na Al-Qaeda,wameuawa katika shambulio lililofanywa na vikosi vya angani vya Marekani.Shambulizi hilo lilifanywa karibu na mji wa Baquba katika wilaya ya Diyala,baada ya helikopta za Marekani kuona kikundi cha watu wenye silaha,kikijaribu kuwakwepa polisi,walipoingia mji wa Khalis.Kama wanajeshi 10,000 wa Marekani na Iraq,wakisaidiwa na helikopta na magari ya kijeshi,wanashiriki katika operesheni kubwa,dhidi ya ngóme za Al-Qaeda katika wilaya ya Diyala.