1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Baraza la mpito nchini Haiti hatimaye kusimikwa

Lilian Mtono
25 Aprili 2024

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Haiti imesema jana kwamba, sherehe ya kulisimika baraza la mpito la urais lililokwama kwa muda itafanyika hii leo katika mji mkuu Port-au-Prince.

https://p.dw.com/p/4f9mr
Haiti yakumbwa na machafuko |
Polisi wa Haiti wakiwa wamesimama kulinda katika mji wa Port au Prince katikati ya machafuko ya magenge ya uhalifu Picha: Clarens Siffroy/AFP

Taarifa hiyo ya ofisi ya Waziri Mkuu anayemaliza muda wake Ariel Henry aidha ilisisitiza kwamba sherehe hiyo itafanyika katika ofisi yake rasmi inayojulikana kama Villa d'Accueil na si kwenye makazi ya rais ya kitaifa ambayo mara kadhaa yameshambuliwa na magenge ya wahalifu.

Mapema jana Jumatano, kiongozi mwenye nguvu wa genge la wahalifu Jimmy Barbeque Cherizier ailisisitiza kwamba mazungumzo juu ya mustakabali wa kisiasa wa Haiti yatatakiwa kuyahusisha magenge hayo. 

Baraza hilo la mpito linalojumuisha wajumbe tisa linachukua madaraka kutoka kwa Henry, lakini limechelweshwa kwa wiki kadhaa kutokana na mvutano wa makundi mbalimbali ya kisiasa juu ya udhibiti.

Kuanzishwa kwa baraza hilo kunachukuliwa kama jambo la msingi na hatua ya kwanza kuelekea kumaliza machafuko ambayo yamelikumba taifa hilo la kisiwa, ambalo kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na magenge hasimu ya wahalifu yanayopigania maeneo, hasa katika mji mkuu.

Soma pia:Zaidi ya watu 50,000 wakimbia mji mkuu wa Haiti

Baraza hilo linatarajiwa kumteua Waziri Mkuu wa muda na kusaidia kuunda serikali ambayo hatimaye itaandaa uchaguzi wa kitaifa.