1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la usalama larefusha muda wa jeshi nchini Iraq.

19 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cdmz

New York.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa limepiga kura kurefusha muda wa kukaa nchini Iraq kwa majeshi ya kimataifa yanayoongozwa na Marekani kwa muda wa mwaka mmoja. Maafisa wa Iraq wamesema kuwa wanamatumaini hii itakuwa mara ya mwisho kuomba kurefushwa kwa muda wa jeshi hilo. Zaidi ya wanajeshi 150,000 wengi wao kutoka Marekani wako hivi sasa nchini Iraq. Balozi wa Iraq katika umoja wa mataifa Hamid al-Bayati amesema kuwa wakati Wairaq wanashukuru kuwa Saddam Hussein ameondolewa madarakani, lakini hawataki tena kuwepo kwa majeshi ya kigeni katika ardhi yao.