1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayer Leverkusen watinga nusu fainali ya Ligi ya Ulaya

19 Aprili 2024

Mabingwa wapya wa Bundesliga, Bayer Leverkusen wametinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya katika mchezo wa kuamkia leo na kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa mechi 44 katika mashindano yote ya msimu huu.

https://p.dw.com/p/4ewuE
Mashabiki wa Bayer Leverkusen wakishangilia bao.
Mashabiki wa Bayer Leverkusen wakishangilia bao.Picha: Hesham Elsherif/Anadolu/picture alliance

Bayer Leverkusen imetoka sare ya 1-1 na West Ham ya Uingereza katika mchezo wa marudiano robo fainali na kupata mabao 3-1 katika michezo yote miwili. Timu hiyo ya Ujerumani itamenyana na Roma kuwania kufuzu fainali.

Soma pia:Bayer Leverkusen yatua London kukwaana na West Ham

Wakati huo huo timu ya Liverpool ya Uingereza imeshindwa kupenya nusu fainali japo kuwa imeshinda mtanange wake wa marudiano kwa bao 1-0  dhidi ya Atalanta ya Italia na kupoteza mabao 3-1 katika michezo yote miwili.