1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bayern wababe tena Ujerumani

20 Mei 2019

Bayern Munich wamelinyakua taji lao la ishirini na tisa la Bundesliga katika siku ya mwisho ya mechi za Ligi Kuu ya Ujerumani baada ya kuiaibisha Eintracht Frankfurt magoli sita kwa moja.

https://p.dw.com/p/3ImCE
Bundesliga 34. Spieltag | FC Bayern München - Eintracht Frankfurt | Meisterschaftsfeier Bayern
Picha: Getty Images/AFP/J. MacDougall

Mechi hiyo ilichezwa katika uwanja wa nyumbani wa Bayern Allianz Arena.

Mustakabali wa kocha Niko Kovac kwa sasa bado haujulikani hapo Bayern licha ya kulibeba taji hilo la Bundesliga na kuweka rekodi ya kuwa mtu wa pili kuebuka bingwa wa taji hilo kama mchezaji na kama kocha baada ya Franz Beckenbauer.

Borussia Dortmund wamemaliza msimu kwenye nafasi ya pili baada ya kupata ushindi wa 2-0 uwanjani Borussia Park walipokuwa wakichuana na wenyeji Borussia Moenchengladbach.

Dortmund walifungiwa mabao yao na Jadon Sancho na nahodha Marco Reus.