1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIJING : Ujenzi wa reli ya kasi wasitishwa

27 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBxt

China imesitsiha ujenzi wa reli mpya ya mwendo wa kasi yeye kutumia nguvu za smaku.

Shirika la habari la serikali la Xinhua limesema mpango huo umefutwa kutokana na malalamiko juu ya uwezekano wa kuwepo na athari za miale ya nuklea kwa wakaazi walio karibu na reli hiyo. Reli hiyo ambayo ilikuwa iunganishe mji wa Shanghai na ule wa Hangzhou ilikuwa iwe reli ya pili duniani kutumia teknolojia ya Ujerumani.

Ya kwanza inaunganisha uwanja wa ndege wa Shanghai na kitovu cha biashara cha mjio huo na teknolojia ya treni hiyo hutumia smaku zenye nguvu kubwa na husafiri kwa mwendo wa kasi wa kilomita 450 kwa saa.