1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Marekani yapeleka msaada wa kijeshi Lebanon

25 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CByL

Ripoti zinasema ndege mbili za mizigo zimewasili uwanja wa ndege wa Beirut nchini Lebanon,zikiwa na misaada ya kijeshi ya Marekani.Msaada huo umeitikia ombi la serikali ya Lebanon.Vikosi vya serikali hiyo vinapigana na wanamgambo wa kundi la Fatah al-Islam,walioidhibiti kambi ya wakimbizi wa Kipalestina,Nahr al-Bared,kaskazini mwa Lebanon.Waziri wa nje wa Marekani,Condoleezza Rice kwa mara nyingine tena amesema,Marekani inaiunga mkono serikali ya Lebanon.Akaongezea kuwa wanamgambo katika kambi ya Nahr al-Bared wanajaribu kuipindua serikali ya kidemokrasia.Kwa upande mwingine,msafara wa magari ya Msalaba Mwekundu umeondoka mji mkuu wa Jordan,Amman, ukipeleka chakula kaskazini mwa Lebanon.