1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT: Mwito wa kutoingilia mambo ya ndani ya Lebanon

3 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCn3

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier ametoa mwito kwa Syria kutambua mamlaka ya Lebanon.Baada ya kukutana na waziri mkuu Siniora mjini Beirut,Steinmeier alisisitiza kuwa mazungumzo yaliopangwa kufanywa siku ya Jumatatu mjini Damaskus yana ujumbe maalum na hayahusiki na upatanisho.Waziri Steinmeier alieleza wazi wazi kuwa Ujerumani itaendelea kuisaidia Lebanon na ziara yake ni ishara ya kuunga mkono uhuru wa Lebanon.Leo,Steinmeier anavitembelea vikosi vya wanamaji wa Kijerumani vinavyolinda mwambao wa Lebanon chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa.Azma ya ujumbe huo,ni kuzuia usafirishaji wa silaha za magendo kwa makundi ya Hezbollah.