1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Beirut.Waziri Gamael aliyeuwawa azikwa hii leo.

23 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCq9

Maelfu ya wa-Lebanon wamekusanyika huko Beirut ili kutoa heshima zao za mwisho kufuatia mauaji ya waziri wa Lebanon Pierre Gamael.

Kundi kubwa la jeshi la Lebanon limewekwa tayari kwenye mji mkuu ili kukabiliana na hali yoyote ya machafuko endapo itatokea.

Muungano wa Gamayel ambao unailaumu Syria kutokana na mauaji hayo, umeitisha maandamano makubwa.

Wakati huo huo, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limethibitisha ombi la serikali ya Lebanon la kufanyia uchunguzi kifo cha waziri huyo.

Uchunguzi huo utafanywa na kamisheni ya Umoja wa Mataifa ambayo tayari ilishafanya uchunguzi wa kifo cha Waziri Mkuu wa Lebanon Rafik Hariri kilichotokea mwaka 2005.

Nae katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amehimiza pawepo mashirikiano na utulivu kutoka nchi zote za eneo hilo.