1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BEIRUT:Waziri mkuu Siniora amshutumu Hassan Nasralla kwa kutaka kuipindua serikali

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CClD

Waziri mkuu wa Lebanon Fouad Siniora amemshutumu kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah kwa kula njama za kutaka kuipindua serikali.

Haya yamekuja baada ya kiongozi wa Hezbollah Nasrallah kuapa kwamba pamoja na wafuasi wake wataendelea na maandamani dhidi ya serikali ya Siniora inayoungwa mkono na nchi za Magharibi.

Maandamano hayo yalianza ijumaa iliyopita ambapo maelfu ya watu wamekuwa wakimiminika majiani mjini Beirut kuipinga serikali.

Upinzani unaolijumusiha kundi la Hezbollaha na makundi mengine yanayoiunga mkono Syria hawaitambui serikali kufuatia kujiuzulu mwezi uliopita mawaziri sita.

Kwa upande mwingine waziri mkuu Fuad Siniora analishutumu kundi la Hezbollah kwa kujaribu kuzuia uchunguzi wa kimataifa kuhusu mauaji ya waziri mkuu wa zamani Rafik Hariri aliyeuwawa mwezi Februari mwaka 2005.