1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Belgrade.Ghala ya silaha ya kijeshi yaripuka chini Serbia.

19 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD1N

Mripuko mkubwa umetokea katika ghala ya silaha ya jeshi la Serbia hii leo, na kuwajeruhi kiasi cha watu 10.

Polisi wamesema mripuko huo umetokea mapema leo katika ghala ya kijeshi karibu na Paracin, kiasi cha kilomita 150 kusini mwa Belgrade, lakini chanzo cha mripuko huo hakijafahamika.

Waziri wa ulinzi wa Serbia Zoran Stankovic amesema ghala hiyo ambayo ilihifadhiwa kiasi kikubwa cha risasi na miripuko imehamishwa baada ya mripuko wa awali.