1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benitez arejesha kumbukumbu Liverpool

Sekione Kitojo
26 Desemba 2018

Kurejea kwa Rafa Benitez katika uwanja wa Anfield katika siku ya Boxing kunatarajia kurejesha kumbukumbu ya changamoto ya Liverpool  ambayo haijapata mafanikio ya taji la Premier League, lakini Klopp analenga wakati huu.

https://p.dw.com/p/3AeRn
Jürgen Klopp
Picha: picture-alliance/dpa/M. Pain

Liverpool ya  Klopp  imetengeneza  mwanya  wa  pointi nne juu  ya  msimamo  wa  ligi  wakati Benitez , meneja  wa  klabu  hiyo  kati  ya  mwaka  2004  na  2010 , anafanya  ziara  pamoja na  timu  yake  ya  Newcastle ambayo  imo  katika  hatari  ya  kushuka  daraja  leo Jumatano (26.12.2012).

Fußball Premier League Huddersfield Town - FC Liverpool 0:1
Dejan Lovren(kushoto) akimkumbatia mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah (kulia)Picha: picture alliance/Actionplus

Kuna  hisia  nzito  kwamba  huu  unaweza  kuwa  msimu  ambao  taji  hilo  la  ligi  ya  England linaweza  kuja  Anfield kwa  mara  ya  kwanza  tangu  mwaka  1990, licha  ya  kuwa  historia ya  hivi  karibuni  inatoa  ujumbe  mchanganyiko  juu  ya  iwapo hicho  kinaweza  kutokea.

Kwanza, habari  nzuri  kwa  Liverpool: Katika  misimu  minane  kati  ya  10  iliyopita, viongozi katika  siku  ya  Krismasi  wameweza  kulinyakua  taji  hilo  la  ligi ya  Premeier.

Na sasa  habari  mbaya: Katika mara  mbili  haikutokea, viongozi  wa  wakati  wa  sikukuu  ya Krismasi  walikuwa  Liverpool.Katika  mwaka 2008/09, Manchester  United ilishinda ubingwa , katika  mwaka  2013/14 ilikuwa  Manchester City.

Jürgen Klopp
Kocha wa Liverpool Juergen KloppPicha: picture-alliance/AP Photo/R. Vieira

Kuanguka  kwa  wakati  huo  na  kushindwa  kupata  ubingwa  mwaka  2014 huenda  ilikuwa maumivu  ya  hivi  karibuni  zaidi kwa mashabiki  wa  Liverpool , lakini  kushindwa  mwaka 2009, chini  ya  Benitez, huenda  kunatoa sababu  zaidi za  kukata  tamaa. Hali  zote zinatoa masomo  kwamba  klabu  hiyo  ya  Merseyside , hata  hivyo, inaonekana  klabu  hiyo imeweza  kuyamudu  mambo  hayo.

Kikosi  cha  Brendan  Rodgers  cha  mwaka  2013 /14 hakikuwa  na uwiano  kama  kikosi cha  sasa  cha  kocha  Klopp.

Wakati Rodgers alikuwa  na  safu  ya  ushambuliaji , ya Luis Suarez akisaidiwa  na  Daniel Sturridge  ambaye  yuko  fiti, kikosi  hicho  kwa  upande  wa  ulinzi  ilikuwa  na  wasi  wasi.

Rafa Benitez Trainer Real Madrid
Kocha wa Newcastle Rafa BenitezPicha: picture-alliance/dpa/B. Alino

Meneja  huyo  wa  Liverpool  alikuwa  na  walinzi wanne , Martin Skrtel, Daniel Agger, Mamadou Sakho na  Kolo Toure,  lakini  alisumbuka  kupata  wachezaji  wawili wa  kwanza. Timu  iliyofunga  mabao 101 ya  ligi  na  kufungwa  mabao  50, ni  mengi  mno  kwa  kikosi  hicho  kuweza  kuwania  kupata  ubingwa.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe