1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Condoleezza Rice ahudhuria mkutano kuhusu Mashariki ya Kati mjini Berlin

21 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQ1

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, yumo mjini Berlin hapa Ujerumani kuhudhuria mkutano wa pande nne zinazoudhamini mpango wa amani ya Mashariki ya Kati.

Condoleezza Rice anatarajiwa kukutana hii leo na waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani, Frank Walter Steinmeier, na kansela wa Ujerumani, Bi Angela Merkel.

Katika mkutano huo, Bi Rice atawaeleza viongozi hao wa Ujerumani juu ya mazungumzo yake na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert na rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas waliyokuwa nayo juzi Jumatatu mjini Jerusalem.

Mazungumzo hayo yalifeli kufikia makubaliano ya maana.