1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Madreva wa treni wagoma kazi saa 30

26 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cj

Nchini Ujerumani,mgomo mpya wa saa 30 uliofanywa na madreva wa treni umeathiri zaidi ya treni 11,000.Kwa mujibu wa shirika la reli la Ujerumani,hasara iliyosababishwa ni kama Euro milioni 10.Madreva wa treni wanadai kuongezwa mshahara kwa asilimia 31,lakini shirika la treni la Ujerumani lipo tayari kutoa nyongeza ya asilimia 10 tu pamoja na malipo ya mara moja ya Euro 2,000.