1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Merkel kujadili katiba ya Umoja wa Ulaya

26 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXh

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anapanga kuwa na mazungumzo mazito ya pande mbili mjini Berlin na nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kati ya tarehe 21 mwezi wa Mei na tarehe Mosi mwezi wa Juni kujaribu kufikia muafaka juu ya katiba mpya ya Umoja wa Ulaya.

Barua ilioandikwa tarehe pili mwezi wa Februari iliotumwa na Merkel kwa viongozi wenzake wa Umoja wa Ulaya imeziomba serikali kuwateuwa wajumbe kujadili katiba hiyo kwa niaba yao katika miezi ya hivi karibuni.

Kwa mujibu ratiba ya mazungumzo hayo ilioambatanishwa kwenye baruwa hiyo mazungumzo ya awali kati ya wajunbe wa Umoja wa Ulaya kujadili azimio la maadili ya Umoja wa Ulaya kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya uliopangwa kufanyika kuanzia tarehe 24 hadi tarehe 25 mwezi wa Machi mjini Berlin yanafanyika wiki hii na wiki ijayo.

Nchi 18 zilizoridhia rasimu ya katiba hiyo iliokwama kuidhinishwa zinatazamiwa kukutaka mjini Madrid Uhispania leo hii kujaribu kuufuwa upya mchakato huo.

Nchi zinazopinga katiba hiyo Uingereza,Ufaransa,Uholanzi, Poland,Jamhuri ya Czech,Denmark na Sweden haizotohudhuria mkutano huo.