1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin: Rais wa kamisheni ya Ulaya, Barosso, amtembelea Kansela Merkel wa Ujerumani mjini Berlin

9 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CBHZ

Katika ziara yake mjini Berlin, mkuu wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Baroso, ameipongeza Ujerumani kwa mchango wake katika kuuweka mswada wa katiba ya Umoja wa Ulaya juu katika ajenda ya harakati zake. Baada ya kufanya mazungumzo na baraza la mawaziri la Kansela Angela Merkel, Bwana Barosso alisema Ulaya iliokuwa kubwa zaidi inahitaji mfumo mpya, licha ya kwamba wapigaji kura wa Ufaransa na Uholanzi waliukataa mswada wa katiba hiyo hapo mwaka 2005. Hadi sasa mataifa 18 kati ya 27 ya Umoja wa Ulaya, ikiwemo Ujerumani, zimeukubali mswada huo wa katiba. Akiutembelea mkoa wa Bavaria hapa Ujerumani, kiongozi wa cham cha Conservative cha Uengereza, David Cameron, ameielezea katiba hiyo kuwa ni hati iliokufa ambayo Ulaya haiihitaji. Bwana Cameron alikuwa anahudhuria mkutano wa cha cha Ki-Conservative cha CSU cha Mkoa wa Bavaria.