1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Uchumi wa Ujerumani kukuwa kwa asilimia 1.7

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYB
Iraq inaendelea kukumbwa na mashambulio
Iraq inaendelea kukumbwa na mashambulioPicha: AP

Serikali ya Ujerumani inatabiri kwamba uchumi wa Ujerumani utakuwa kwa kiwango cha asilimia 1.7 katika mwaka huu wa 2007.

Rasimu ya repoti mpya ya kiuchumi ya kila mwaka itakayotolewa baadae mwezi huu pia inatarajia ukosefu wa ajira kupunguwa kwa takriban watu laki tano ikiwa ni sawa na asilimia 12 ya kupunguwa kwa kiwango cha ukosefu wa ajira.

Utabiri wa serikali unakuwa wa hadhari zaidi kulinganisha na ule wa makampuni ambao umekuwa wa matumaini zaidi juu ya matarajio ya ukuaji wa uchumi wa Ujerumani.