1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN : Vipaza sauti vyagundulika ofisi ya bunge

24 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYO
Jengo la Bunge la Kenya jijini Nairobi
Jengo la Bunge la Kenya jijini NairobiPicha: DW

Kugunduliwa kwa vipaza sauti viwili katika ofisi ya mbunge wa Ujerumani mjini Berlin kumezusha hofu ya kuibuka kwa kashfa ya kudukiza habari kwa siri.

Gazeti la Stuggarter Nachrichten limesema wataalamu wa usalama wameanza akaguzi katika ofisi za wabunge wa bunge la Ujerumani Bundestag ambao wako kwenye kamati ya bunge yenye kusimamia shughuli za ujasusi.Vipaza sauti hivyo viliyowekwa juu ya taa viligundulikana Ijumaa iliopita katika ofisi ya mjumbe wa kamati hiyo Wolfgang Neskovic wa chama cha Left cha mrengo wa shoto.

Maafisa utawala katika bunge la Ujerumani wamesema vipaza sauti hivyo vilikuwa ni vya kawaida na havifai kwa shughuli za kudukiza habari.