1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Wajerumani wapinga ujenzi wa msikiti

3 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCdu

Wajerumani takriban 50 jana walifanya maandamano kupinga kuanza kwa ujenzi wa msikiti wa kwanza katika eneo la mashariki mwa Ujerumani. Maofisa 90 wa polisi walitumwa katika wilaya ya Pankow-Heinersdorf kulinda usalama. Msemaji wa polisi, Marcel Kuhlmey, amesema maandamano hayo yalifanyika kwa amani licha ya waandamanaji kuwa na hasira.

Msikiti huo unadhaminiwa na jamii ya waislamu ya Ahmadiyya iliyo na wafuasi 30,000 nchini Ujerumani. Inakadiriwa waumini takriban 200 wanaishi katika mji mkuu Berlin.

Wakaazi wa eneo kunakojengwa msikiti huo wamekasirishwa wakilalamika kwamba hawakushauriwa kuhusu ujenzi wa msikiti huo na wala hakuna muislamu yeyote wa Ahmadiyya anayeishi katika eneo hilo.