1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Berlin. Wanasiasa wataka jeshi la Ujerumani kutowekwa nchi za nje.

29 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCy3

Wanasiasa wawili waandamizi nchini Ujerumani wametoa wito wa kufikiri upya juu ya uwekaji wa majeshi ya Ujerumani, Bundeswehr nje ya nchi hiyo.

Waziri wa ulinzi Franz Joseph Jung ameliambia gazeti la Frankfurter Allgemeine linalotolewa kila Jumapili kuwa ujumbe wa jeshi la Ujerumani unapaswa kufanyiwa tathmini dhidi ya uwezo wake wa utendaji.

Jung amesema idadi kubwa ya wabunge ina wasi wasi kuwa jeshi hilo limefikia kikomo.

Mtangulizi wa Jung na kiongozi wa sasa wa bunge katika kundi la wabunge wa chama cha Social Democrats Peter Struck , amedai kuwa ujumbe wa Bundeswehr upunguzwe kwa mfano nchini Bosnia na Kosovo.