1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN: Waziri Steinmeier atatoa ushahidi wake mwezi Machi

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCW1

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier anatazamiwa kutoa ushahidi wake tarehe 8 mwezi Machi,mbele ya kamati ya uchunguzi ya idara ya upelelezi ya Ujerumani BND.Uchunguzi huo unahusika na mkasa wa raia wa Kituruki aliezaliwa Ujerumani,Murat Kurnaz ambae alizuiliwa katika jela ya kijeshi ya Marekani huko Guantanamo Bay.Kwa mujibu wa mjumbe mmoja wa kamati hiyo ya uchunguzi,hata waziri wa ndani wa zamani wa Ujerumani,Otto Schilly ameombwa siku hiyo aende kutoa ushahidi wake.Kamati hiyo itakutana mara tatu kabla ya kumhoji waziri Steinmeier.Inasemekana kuwa wajumbe wa sheria na idara ya upelelezi,wa ngazi ya juu,watahojiwa katika kikao maalum mwisho wa mwezi wa Februari.Joschka Fischer ambae hapo zamani alikuwa waziri wa masuala ya nchi za nje, ataalikwa pia hapo tarehe mosi mwezi Machi.