1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN.Donald Rumsfeld afunguliwa mashtaka nchini Ujerumani

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsc

Asasi za kutetea haki za binadamu za nchini Ujerumani zimeandaa mashtaka dhidi ya aliyekuwa waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld na maafisa wengine wa ngazi za juu katika wizara hiyo.

Watetea haki hao wanadai kwamba waziri huyo na maafisa wake waliidhinisha mateso ya wafungwa kwenye jela ya Abu Ghraib nchini Irak na katika jela ya Guantanamo.

Wanasheria wa Ujerumani na Marekani wameamua kufungua mashtaka hayo nchini Ujerumani kwa mujibu wa sheria inayoruhusu kumuhukumu mtu yeyote anaetenda uhalifu wa kivita popote pale duniani.

Mashtaka hayo yametayarishwa kwa niaba ya raia 11 wa Irak waliofungwa kwenye jela ya Abu Gharib na mtu mmoja aliewekwa mahabusu katika jela ya jeshi la Marekani ya Guatanamo.