1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Marufuku ya uvutaji sigara yaanza

1 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBdE

Upigaji marufuku uvutaji wa sigara unaanza kutumika leo hii katika mikoa mitatu kati ya 16 nchini Ujerumani.

Marufuku hiyo inatumika katika hospitali,shule na majengo ya serikali katika mkoa wa Baden-Württermberg,Lower Saxony na Mecklenburg-West Pomerania.

Uvutaji sigara pia umepigwa marufuku katika mikahawa na vilabu vya pombe katika mikoa miwili ya Baden-Württenberg na Lower Saxony venginevyo kunakuwepo na chumba maalum cha kuvutia sigara.

Hatua hiyo ya mikoa mitatu inakuja mwezi mmoja kabla ya marufuku ya taifa kwa uvutaji sigara kwenye majengo ya serikali,usafiri wa umma na taxi kuanza kufanya kazi.

Ujerumani imekuwa ikijadili upigaji marufuku uvutaji wa sigara kwa miaka kadhaa lakini hatua zake hizo hazilingani sana na kupigwa marufuku moja kwa moja kwa uvutaji sigara kulikoamuriwa na nchi nyingi jirani za Umoja wa Ulaya.