1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BERLIN:Mpango wa kitaifa ni hatua muhimu

12 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBjP

Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel anaelezea mpango wa kitaifa wa kuwajumuisha raia wa kigeni katika jamii hapa Ujerumani kuwa hatua muhimu.Bi Merkel aliyasema hayo katika mkutano rasmi na wawakilishi wa uhamiaji ili kuimarisha hatua ya kuwajumuisha raia wa kigeni hapa Ujerumani.Hata hivyo makundi machache ya raia wa Uturuki wameamua kususia kikao hicho kufuatia kupitishwa kwa sheria mpya ya uhamiaji inayowalazimu mke au mume wa raia wa kigeni aliye na kibali cha kubaki Ujerumani kuwa na ujuzi wa lugha ya Kijerumani kabla kuruhusiwa kuingia nchini.

Yapata watu 90 wanatarajiwa kuhudhuria kikao hicho ambacho ni cha kwanza cha aina hiyo kufanyika.Bi Merkel alianzisha mpango wa kitaifa wa kuwajumuisha raia wa kigeni katika jamii mwezi Julai mwaka jana.Baraza la mawaziri la Ujerumani hapo jana liliidhinisha matumizi ya euro milioni 750 kila mwaka ili kufanikisha mpango huo.Mpango huo unalenga kuimarisha masomo ya lugha ya kijerumani kwa raia wa kigeni.

Kulingana na serikali takriban watu milioni 15 wanaoishi hapa Ujerumani wana asili ya mataifa ya kigeni.Yapata watu milioni 2.6 walio na asili ya Uturuki waanishi hapa Ujerumani.