1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bernard Membe, Tanzania

23 Mei 2013

Bernard Membe ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania. Bwana huyu mwenye umri wa miaka 60 anatambua changamoto zilizoko, lakini pia ufanisi wa Umoja wa Afrika.

https://p.dw.com/p/18c9y
Aussenminister Tansania Bernard Membe
Aussenminister Tansania Bernard MembePicha: Getty Images

"Katika kipindi cha miaka 50, mataifa yote 54 ya Kiafrika sio tu yamejishughulisha na ukombozi wa kisiasa bali pia wa kiuchumi. Changamoto katika kipindi hicho cha miaka 50 zilikuwa nyingi na tofauti. Kwa mfano kurejea desturi mbaya za kunyakuwa madaraka kupitia mapinduzi. Halafu,vita vya wenyewe kwa wenyewe: Tuna matatizo makubwa nchini Somalia na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tunaona lakini pia kuna juhudi za kimataifa kuipatia ufumbuzi mizozo hiyo. Miaka 50 ya Umoja wa Afrika inatukumbusha Tanzania na mchango mkubwa wa nchi yetu na serikali yetu chini ya uongozi ya muasisi na baba wa taifa letu, marehemu Mwalimu Julius Nyerere."