1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biashara ya vifaa vya ulinzi yanawiri Ujerumani na Kimataifa

6 Desemba 2010

Ugaidi,Uhalifu,Uharamia,na Uhalifu ndio chanzo kikuu cha kushamiri biashara hiyo

https://p.dw.com/p/QQYn
Waziri wa Uchumi Rainer BruederlePicha: AP

Ujerumani ni mojawapo ya nchi zinazotajwa kuwa bingwa wa kusafirisha bidhaa nje,lakini sasa taji hilo inabidi kuiachia China.Hata hivyo haina maana kwamba Ujerumani imeondoka katika orodha ya nchi zinazosafirisha bidhaa nje.Vitu ambavyo zaidi vinatoka Ujerumanivilivyo na soko kubwa nchi za nje ni pamoja na Magari,mashine na kemikali zinazotengenezwa humu nchini.Juu ya hilo lakini sasa biashara inayoonekana kunawiri zaidi ni ile ya vifaa vya ulinzi wa usalama,kama ving'ora,milango na kadhalika.Kuvuma kwa biashara hiyo Ujerumani ni kutokana na kuongezeka kitisho cha ugaidi pamoja na uhalifu wa kupangiliwa.Serikali ya Ujerumani sasa imeanzisha mradi maalum wa kusafirisha bidhaa hizo.

Saudi Arabia imeweka mpaka wa kilomita 9000 baina yake na majirani zake.Katika eneo hilo la mpaka nchi hiyo ya kifalme imejizatiti kiusalama kwa kuweka mifumo ya Rada,nyaya za umeme,kamera pamoja na vifaa vingine maalum vya kuchunguza mienendo mipakani na kuweka usalama.Hiyo ni biashara ambayo imeingiza kiasi cha Euro billioni  mbili.Faida iliyotokana na biashara hiyo imeuangukia muungano wa makampuni ya Ujerimani.Makampuni hayo ni pamoja na kampuni tanzu ya Ulaya inayohusika na biashara ya silaha ya EADS iliyo na makao makuu yake mjini Munich.Holger Mey ambaye ni anahusika na masuala ya mikakati katika kampuni hiyo anasema biashara hiyo haiwezi kufanikiwa ikiwa hapatokuwepo uungaji mkono wa kisiasa.

'' Soko la vifaa vya usalama sio soko huru hata kidogo,haiwezekani kuifanya biashara hiyo kila mahala kwa uhuru.Kuna wateja wengi wa kisiasa ambao wanafanya kutokana na mtazamo wa kisiasa na mtazamo huo sio mara zote unaangalia kigezo cha kutoa soko.Hata hapa kwetu kuna uungaji mkono wa kisiasa katika biashara hii ya vifaa vya usalama na mara nyingi ni utawala ndio unaoamua kuhusu kufuatilia biashara fulani.``

Biashara ya silaha na vifaa vya usalama isingeweza kufanikiwa wakati huu kama sio kuongezeka kitisho juu ya masuala ya ugaidi,uhalifu wa kupangwa,uharamia,majanga ya kiasili.Ulimwengu unatengeneza kiasi cha Euro Billioni 100  kutokana na biashara ya technologia ya usalama kwa ajili ya majengo,na njia za usafiri,au vyombo vya mawasiliano.Kila mwaka mahitaji hayo yanaongezeka kwa asilimia 5.Ujerumani pekee inatarajia kufikia mwaka 2015 kuongeza kipato chake hadi Euro billioni 31  kutokana na biashara hiyo.Tayari waziri wa uchumi nchini Rainer Brüderle amependekeza kuanzisha mradi wa kusafirisha  bidhaa aina hiyo katika masoko ya kimataifa anasema.

''Soko la Technologia ya usalama inaweka matumani ya muda mrefu ya  kukua kwa uchumi wetu.Hii ni kusema kwamba hali hii haiwezi kuhatarisha uchumi wetu.Sote tuna uhakika  wa jambo hili,kwamba hatari ni ndogo mno na ndio sababu tunaangalia zaidi kuhusu usalama .Lakini kabla hatujafikia umbali huo ni lazima kwa maslahi yetu ya usalama tuone nafasi ya masoko.Chini ya mradi huu wa ''usalama uliotengenezwa Ujerumani'' tutajiwekea nafasi nzuri ya kuupiga jeki mradi huo''

Kutokana basi na mkakati huo ndio sababu kwa hivi sasa kuna jitihada nyingi za kujongeleana mataifa pamoja na kuweko makubaliano ya kisiasa  kati ya serikali mbali mbali.Hivi karibuni ujumbe wa Ujerumani utafanya ziara kuanzia huko India hadi falme za kiarabu kwa lengo la kuutia msukumo mradi huo.

Mwandishi:Kinkartz Sabine/Saumu Yusuf

Mhariri: M. AbdulRahman.