1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden aahidi kuilinda Ufilipino kwenye bahari ya Kusini

12 Aprili 2024

Rais Joe Biden wa Marekani ameapa atailinda Ufilipino dhidi ya shambulio lolote katika eneo la bahari ya kusini mwa China ambalo limekuwa kitovu cha mvutano mkubwa kati ya serikali mjini Manilla na utawala mjini Beijing.

https://p.dw.com/p/4egtJ
Joe Biden
Rais wa Marekani Olaf Scholz Picha: Andrew Harnik/Getty Images

Biden ametoa ahadi hiyo usiku wa kuamkia leo wakati alipowakaribisha ikulu mjini Washington rais Ferdinand Marcos Jr. wa Ufilipino na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida kwa mkutano wa ngazi ya juu wa nchi hizo washirika.

Amesema ahadi ya Marekani ya kutoa ulinzi kwa Japan na Ufilipino ni thabiti na kuongeza kuwa Washington itaisaidia Ufilipino iwapo kutatokea shambulio lolote dhidi ya meli, ndege au vikosi vya nchi hiyo kwenye bahari ya kusini mwa China.

Biden aapa kuzilinda Ufilipino na Japan katikati mwa mvutano na China

Mkutano wa viongozi hao wawatu umefanyika katikati mwa makabiliano yanayoongezeka kati ya meli za Ufilipino na China katika eneo hilo la bahari lenye mzozo ambalo Beijing inadai kulimiliki.