1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Biden kutohudhuria Mkutano wa kilele wa COP28

Saumu Mwasimba
27 Novemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden hatoshiriki mkutano wa kilele kuhusu mazingira utakaofanyika Dubai wiki hii.

https://p.dw.com/p/4ZU4x
VAE, Abu Dhabi | #COP28 Aufsteller
Rais Joe Biden hatohudhuria mkutano wa COP28.Picha: Amr Alfiky/REUTERS

Wajumbe takriban 70,000 wakiwemo viongozi wa nchi pamoja na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Papa Francis wanatarajiwa kushiriki mkutano huo wa COP28 utakaofunguliwa alhamisi ambao huenda ukawa ndio mkutano wa kilele mkubwa zaidi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira kuwahi kufanyika.

Soma pia: Wataalam wa Afya: Watetezi wa nishati ya visukuku wasishiriki COP28

Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu sababu za Rais Biden kutohudhuria COP28. Kwa mujibu wa afisa mmoja aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, serikali ya Biden bado iko kwenye majadiliano kuhusu ikiwa itatuma afisa wake wa ngazi ya juu kwenye mazungumzo hayo ya Dubai.

Mjumbe anayehusika na mazingira nchini Marekani na aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje  John Kerry ataongoza mashauriano ya  kila siku kwa niaba ya nchi hiyo.