1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BLANTYRE:Wilaya tano kukabiliwa na uhaba wa chakula

13 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7G9

Shirika la chakula la umoja wa mataifa WFP limetowa taarifa kwamba takriban watu laki tano na elfu ishirini katika wilaya nne nchini Malawi ambazo zimeathirika vibaya na ukame wamo katika hatari ya kukabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula kabla ya msimu wa mavuno wa mwaka ujao wa 2008.

Wilaya hizo ni pamoja na wilaya za Karonga na Mzimba zilizo kaskazini wilaya ya kati ya Ntchsi na wilaya ya Mulange iliyo kusini.

Malawi ambayo kwa mwaka inahitaji tani milioni mbili za mahindi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani haikuweza kufikia kiwango hicho kutokana na ukosefu wa mvua na pia mbolea.

Malawi mwaka huu imezalisha tani milioni moja nukta moja pekee za mahindi na kati ya hizo tani laki nne zimepelekwa nchini Zimbabwe.