1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Blinken akutana na rais wa China Xi Jinping mjini Beijing

Amina Mjahid
26 Aprili 2024

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na mwenzake wa China Wang Yi mjini Beijing na kujadili hatua ya China inayopingwa ya kuiunga mkono Urusi.

https://p.dw.com/p/4fDID
Rais wa China Xi Jinping na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Bliken
Rais wa China Xi Jinping na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony BlikenPicha: Mark Schiefelbein/REUTERS

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken amekutana na mwenzake wa China Wang Yi mjini Beijing na kujadili hatua ya China inayopingwa ya kuiunga mkono Urusi, katika vita vyake dhidi ya Ukraine, mgogoro wa Taiwan pamoja na masuala ya biashara.

Wawili hao pia wamejadili juhudi za kuendelea kuimarisha mahusiano yao. Katika mkutano wao uliodumu kwa zaidi ya saa tano, Wang amesema mahusiano kati yao yanaendelea kuwa thabiti, lakini bado wanatofautiana katika mambo fulani na hilo linafanya mazungumzo kati yao kuwa magumu.

Baadae Blinken alikutana na Rais wa China Xi Jinping aliyemwambia kwamba ni muhimu kwa mataifa hayo mawili kuwa washirika kuliko maadui. Amesema bado kuna masuala kadhaa ya kusuluhishwa na bado kuna muda wa kufanya hivyo.