1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bobi Wine azindua chama kipya cha siasa kabla ya uchaguzi

22 Julai 2020

Mwanaharakati  wa Uganda Bobi Wine amezindua chama kipya cha siasa  kabla ya uchaguzi mkuu  wa rais ambamo  ana  matumaini  kuwa taswira ya umoja  wa upinzani dhidi ya  rais wa  muda  mrefu  nchini  humo Yoweri Museveni.

https://p.dw.com/p/3fhTk
Bildergalerie Persönlichkeiten 2020 | Bobi Wine
Picha: Getty Images/L. Dray

Mwanaharakati  wa  Uganda  Bobi Wine amezindua chama kipya cha  siasa  kabla ya  uchaguzi mkuu  wa  rais ambamo  ana  matumaini  kuwa  taswira  ya  umoja  wa upinzani dhidi ya  rais wa  muda  mrefu  nchini  humo Yoweri Museveni.

Mwanamuziki  huyo maarufu nchini  Uganda  na  mbunge, ambaye  jina  lake  halisi ni Kyagulanyi Ssentamu, ameongoza  kundi la  kutoa  shinikizo  la  kisiasa linalojulikana  kama  People Power, ikiwa  na  maana  ya Nguvu  ya  Umma, ambalo  limevutia  hisia  za  Waganda wengi  kwa  wito  wake  wa  kutaka  rais Yoweri  Museveni kung'atuka.

Je chama kipya cha Bobi Wine kitaleta ushindani Uganda?

Wine  amekiita  chama  chake  kipya  National  Unity Platform, ama  Jukwaa  la  Umoja  wa  Taifa,  na  mwamvuli ikiwa  ndio  nembo  yake. Amekuwa  akitoa  wito  wa  umoja wa  upinzani  dhidi  ya  Museveni, mshirika  wa  marekani katika  usalama  wa  kikanda  ambaye  ameliongoza  taifa hilo  la  Afrika  mashariki  tangu kuchukua  madaraka  kwa njia  ya  kijeshi mwaka  1986.