1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Boko Haram wauwa tena Maiduguri

Mohammed Khelef
8 Agosti 2019

Washambuliaji wawili wa kujitoa muhanga wamewauwa watu watatu kwenye shambulio linalodhaniwa kuwa limefanywa na kundi la kigaidi la Boko Haram katika eneo la kaskazini mashariki mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/3NYea
Nigeria 65 Menschen von Islamisten der Gruppe Boko Haram getötet
Picha: AFP/A. Marte

Watu wengine wanane walijeruhiwa kwenye mashambulio mawili yaliyotokea katika mji wa Mafa ulio kilomita 50 kutoka kwenye mji wa Maiduguri ambao ni mji mkuu wa jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Mkuu wa kitengo cha usalama wa jimbo la Borno, Bello Danbatta, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba washambuliaji hao waliingia kwenye mji wa Mafa wakiwa miongoni mwa wanawake waliokuwa wamekwenda kutafuta kuni.

Kundi la Boko Haram linaloshukiwa kuhusika na mashambulio hayo limekuwa linafanya mashambulizi kwa kipindi cha miaka kumi sasa katika eneo hilo la kaskazini mashariki mwa Nigeria na mara nyingi limekuwa linawatumia wanawake  kuanya mashambulio ya kujitoa mhanga katika maeneo kama vile misikiti, masoko na kwenye vituo vya usafiri.